Picha zaidi ya mripuko brussels uliotokea punde
Kwenye
vyombo vya Habari vya kimataifa, habari inayomake headline sasa hivi ni
taarifa ya mlipuko uliotokea uwanja wa ndege na watu zaidi ya 10
wanakadiriwa kufa na wengine 35 kujeruhiwa.
Uwanja
wa ndege wa Brussels wametoa taarifa kupitia ukurasa wao wa Twitwer na
wamesema kwamba kumekuwa na milipuko miwili na pia shughuli zote za
uwanja wa ndege zimesimama na majengo yameondolewa na milipuko na pia
wameomba watu wasiende maeneo ya uwanja huo. Mpaka sasa haijabainika
chanzo cha milipuko hiyo ambapo vyombo vya habari vya kimataifa vinasema
kuwa milipuko hiyo imetokea siku chache baada ya kukamatwa kwa mshukiwa
wa mashambulio ya Paris mwaka jana ambayo yalisababisha vifo vya watu
130.
No comments:
Post a Comment