Monday, March 28, 2016

WAPIGA NDUMBA KIKWAZO CHA MAENDELEO , KYELA


Mkuu wa wilaya ya Kyela mkoani Mbeya Dkt Thea Ntara ameliagiza jeshi la polisi wilayani humo kufanya msako na kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo vya kupiga ramli kwa madai kuwa wamekuwa wakikwamisha jitihada za serikali za kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.

Akitangaza kuingia tena kwa ugonjwa huo katika taarafa ya Unyakyusa wilayani humo Dokta Ntara amesema kuwa unatokana na kukithiri kwa uchafu katika tarafa hiyo na sio kwa njia ya kurogwa kama ambavyo waganga wa kienyeji na wapiga ramli wanavyowaaminisha wananchi.

Katika hatua nyingine Dokta Ntara ameziomba taasisi za dini kushirikiana na serikali kutoa elimu kwa wananchi namna ya kujikinga na ugonjwa huo.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment