Friday, March 11, 2016

TUNAFUATILIA MKUTANO WA MAJI MAREFU



Wakazi wa Magila Gerezani kata ya Mombo Wilayani Korogwe  Mkoani Tanga wakifuatilia  moja ya mikutano ya Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM) Stivin Ngonyani, maarufu Majimarefu aliyoifanya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kwa kipindi cha pili cha Ubunge.
Mbunge huyo amekuwa aikipita katika kata moja baada ya moja kuwashukuru wapiga kura wake na kusema kuwa uchaguzi umeshapita na Mbunge kupatikana hivyo yeyey ni Mbunge wa wote na kuwataka kufanya kazi kwa pamoja.
Amesema yuko tayari kusikiliza kero na matatizo ya wananchi muda wowote hivyo kusema kuwa ofisi yake iko wazi na kutoa fursa kusema na kutoa kero za wananchi wanazokabiliana nazo




Kwa habari , matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment