Sare dhidi ya Liverpool, inaifanya Man United isubiri hadi mwakani kucheza michuano ya Ulaya
Usiku wa March 17 michuano ya UEFA Europa Ligi iliendelea kama kawaida kwa michezo nane kupigwa barani Ulaya, stori kubwa ilikuwa ni mchezo wa marudiano kati ya Man United dhidi ya Liverpool, ambapo safari hii Man United walikuwa nyumbani.
Mchezo wa kwanza Man United walikubali kichapo cha goli 2-0 kutoka kwa Liverpool ambao wao walikuwa katika uwanja wao wa Anfield, licha ya kuwa kuna usemi unasema mcheza kwao utunzwa, Man United imeshindwa kusonga mbele michuano hiyo.
Baadhi ya watu walikuwa na imani na Man United kuwa wangeweza kubadili matokeo Old Trafford, mtazamo ambao ulianza kuleta dalili njema dakika ya 32, baada ya Anthony Martial kuifungia Man United goli la uongozi kwa mkwaju wa penati, lakini dakika 13 baadae Philippe Coutinho akaisawazishia Liverpool goli.
Hadi dakika 90 zinamalizika Man United na Liverpool ziliambulia sare ya goli 1-1, hivyo kwa matokeo hayo Man United wanaaga rasmi michuano hiyo kwa kufungwa jumla ya goli 3-1. Kwa sasa Man United itasubiri hadi msimu ujao ili icheze mashindano ya Ulaya.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment