Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigellah, akizungumza na wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na wakuu wa Idara mbalimbali Tanga, mara baada ya kukabidhiwa Ofisi na mtangulizi wake, Mwantumu Mahiza leo.
Pamoja na mambo mengine Mkuu huyo wa Mkoa alisema kipindi chake chote atafanya kazi na watu wanaotaka kufanya kazi na hatmvulia mtu yoyote ambaye atakuwa kikwazo cha maendeleo.
Alisema kipindi cha kazi atafanya kazi na hatokuwa rafiki wa mtu ambaye hataki kufanya kazi hivyo kuwataka watendaji na wakuu wa Idara kufanya kazi kwa weledi na kuacha kukaa maofisini kupiga soga.
Alisema yale yote ambayo yamechwa na mtangulizi wake atayaendeleza na yeye kutilia mkazo hivyo kuwataka kumuunga mkono wananchi na watendaji ili kuinua uchumi wa Tanga na kipato cha mtu mmoja mmoja.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment