Friday, March 18, 2016

SIMBA YAJIFUA MKWAKWANI KUMENYANA NA COASTAL KESHO

 Wachezaji wa Simba Sports Club ya jijini Dar es Salaam, wakifanya mazoezi uwanja wa Mkwakwani jioni hii kujindaa na kumenyana na Coastal Union ya Tanga kesho uwanja huo huo wa Mkwakwani.
Timu hiyo ambayo inadaiwa kuingia jijini Tanga saa 5 kamili kwa usafiri wa Pipa walishuka uwanjani hapo na kwenda moja kwa moja hadi katika hoteli waliyofikia.
Ilipofika saa 9, 30 waliingia uwanja wa Mkwakwani kwa kufanya mazoezi huku washabiki wakiwa wamejazana nje ya uwanja baada ya kupata taarifa ya kufika timu hiyo uwanjani hapo kwa mazoezi.




No comments:

Post a Comment