Wednesday, March 30, 2016

ABIRIA WA NDEGE APIGA PICHA MTU ANAEDAIWA KUWA MTEKAJI

Selfie ya Egyptair

Mtu aliyepiga picha na anaedaiwa kuwa mtekaji  wa ndege ya kampuni ya EgyptAir aliyevalia mkanda bandia wa mlipuaji wa kujitolea muhanga amesema kuwa alitaka kuuona vizuri ukanda huo.

Picha hiyo ya Ben Innes ,akitabasamu karibu na mtuhumiwa huyo katika ndege hiyo ya EgyptAir imesambazwa katika mitandao ya kijamii.

  Innes anayeishi Aberdeen pia aliliambia gazeti la Jumapili la Sun kwamba alitaka kuonyesha tabasamu mbele ya shida.

Alisema kuwa picha hiyo iliochukuliwa na mfanyikazi mmoja wa ndege hiyo ilikuwa ''selfie bora zaidi''.

Ndege hiyo ilikuwa ikibeba abiria 55,ikiwemo raia 26 wa kigeni waliotoka Alexandria kueleka Cairo.

Wengi wa wale waliokuwa wameabiri ndege hiyo waliwachiliwa baada ya ndege hiyo kutua katika uwanja wa ndege wa Lanarca lakini mtekaji huyo aliwazuia watu saba kabla ya kisa hicho kukamilika kwa amani.

No comments:

Post a Comment