Sunday, March 13, 2016

AWADHI JUMA AIOKOA SIMBA UWANJA WA TAIFA


Awadh Juma (mbele) akipongezwa na wachezaji wenzake Mussa Mgosi (kulia) na Danny Lyanga (kushoto) baada ya kuifunga bao lililoipa Simba pointi tatu.

Simba bado imeendelea kutamba kwenye ligi ya Vodacom Tanzania bara baada ya kuinyamazisha Tanzania Prisons ya Mbeya kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa raundi ya pili ya ligi uliochezwa kwenye uwanja wa taifa.
 Awadh Juma (katikati) akisujudu baada ya kupachika bao lililoipa Simba ushindi.

Bao pekee lililoipa pointi tatu Simba limewekwa kambani dakika ya 86 na kiungo Awadh Juma kwa shuti kali akiwa nje ya box la 18 na kupeleka shangwe mtaa wa Msimbazi, Kariakoo.

Takwimu muhimu unazotakiwa kuzifahamu
Hamisi Kiiza akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Tanzania Prisons wakati wa mchezo wao wa marudiano kwenye ligi ya Vodacom.


  • Simba wameshinda mchezo wa tatu mfululizo baada ya kufungwa na Yanga bao 2-0. Imeshinda 2-0 dhidi ya Mbeya City, ikaifunga 3-0 Ndanda FC kabla ya leo kuilaza Tanzania Prisons kwa bao 1-0.
  • Jackson Mayanja amefanikiwa kupata ushindi wake wa 9 katika mechi 10 ambazo amesimama kama kocha akikiongoza kikosi cha Simba baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Dylan Kerr.



  • Timu zote zimepata ushindi kwenye michezo yake ya nyumbani msimu huu. TZ Prisons waliifunga Simba kwa bao 1-0 kwenye uwanja wao Sokoine, Mbeya. Simba nao wamepata ushindi kama huo kwenye uwanja wanaoutumia kama uwanja wao wa nyumbani.

Wachezaji wa Simba wakimlaki Awadh Juma baada ya kufunga bao na kuihakikishia timu yake kupata pointi tatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya TZ Prisons

  • Simba wamefunga magoli kuanzia dakika ya 70 na kuendelea kwenye mechi mbili mfululizo. walifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City na leo dhidi ya Tanzania Prisons.

Michezo mingine iliyochezwa March 13 kwenye viwanja vingine matokeo yake yapo kama ifuatavyo.

Majimaji 1-0 Stand United
Kagera Sugar 3-0 Coastal Union
Mgambo JKT 1-1 Mwadui FC

No comments:

Post a Comment