Mkuu wa mkoa Paul Makonda kaanza kazi Dar… maagizo ya kwanza ni haya
Jana March 15 2015 Rais John Pombe Magufuli
aliwaapisha wakuu wapya wa mikoa 26 ya Tanzania bara na kuwaagiza
kutekeleza wajibu wao bila kuwa na hofu yoyote kutoka kwa watu ikiwa ni
pamoja na kuwashughulikia watendaji wote watakaoonekana kuwa wazembe
kwenye sekta zao, leo Marh 16 2016 ndio mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekabidhiwa rasmi ofisi ili kuuongoza mkoa wake.
Licha ya hayo yote Makonda alipata
time ya kufahamiana na baadhi ya watendaji katika ofisi yake, na
hapohapo akatoa agizo la kuwataka wakuu wote wa idara kumfikishia ripoti
zao ikiwa ni pamoja na changamoto zinazowakabili ndani ya saa 24.
‘Tumeingia
kwenye awamu nyingine ya kuongoza mkoa unaojulikana kama Dar es salaam
lakini ukiwa na wilaya tano, sio kazi ndogo, natakiwa kuwa na wilaya
mpya mbili ambazo kwa mara ya kwanza napata nafasi ya kuona namna gani
zikianzishwa ‘
‘wananchi
wanashida ya maji, barabara, matibabu, migogoro ya ardhi nakadharika,
lakini waliamini kumpa majukumu Rais Magufuli ili awatatulie changamoto
hizo‘ ;-Paul Makonda
‘Rais
huyo kaamua kwa Dar es salaam amkabidhi majukumu hayo Makonda ili
aifanye hiyo kazi, Sasa ninawataka wakuu wote wa idara ndani ya saa 24
mnipatie ripoti ya kila idara mliyonayo‘ ;-Paul Makonda
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment