Obama alivyoweka Historia ya mahusiano ya Marekani na Cuba
Baada ya
kutokuwa na uhusiano mzuri kati ya Marekani na jirani yake Cuba kwa muda
mrefu, March 20 2016 Rais Barack Obama amefanya ziara ya siku 3
inayolenga kurekebisha uhusiano wao na Cuba huku Cuba inataka
kuondolewa zaidi vikwazo vyote vya kiuchumi na Marekani.
Rais
Barack Obama amewasili na Air Force one Jumapili ikiwa ni Rais wa
kwanza kutembelea Cuba tangu Calvin Coolidge ambaye alitembelea kwa vita
mwaka 1928.
Rais
Barack Obama ametembelea kwenye mji wa kale wa Havana na pia
aliwahutubia wafanyakazi wa ubalozi mpya wa Marekani na
amesema…>>>‘imekuwa
ni miaka 90 toka Rais wa Marekani kufika hapa Cuba, ni maajabu kuwa
hapa. Mwaka 1928 Rais Coolidge alikuja kwenye vita, ilimchukua siku
tatu kuwa hapa, imenichuka masaa matatu tu kuwa hapa, kwa mara ya kwanza
Air force one imetua Cuba na hii ni hatua ya kwanza na fursa ya
kihstoria kushirikiana na watu wa Cuba‘:-Barack Obama
No comments:
Post a Comment