WAFANYABIASHARA WA MAFUTA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA UWEKEZAJI WA BOMBA LA MAFUTA TANGA HADI UGANDA.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Justin Ntalikwa akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Bomba la Gesi
litakalokuwa likisafirisha kutoka Tanga kwenda uganda.
Mwenyekit wa Chama cha wafanyabiashara wa mafuta nchini(NICOL),
Gidion Kaunda akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam mara baada ya Katibu mkuu kuzungumzia bomba la mafuta la Tanga
kwenda Uganda.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Justin Ntalikwa(aliye mbele) jijini Dar es Salaam leo.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini, Profesa Justin Ntalikwa amesema kuwa wafanyabiahara wa mafuta
wanafursa mbalimbali katika ujengaji wa bomba la mafuta kutoka Tanga
hadi Uganda.
Akizungumza leo na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam, Profesa Ntalikwa amesema kuwa bomba la mafuta
likianza mchakato wafanyabiashara wanaweza kuomba zabuni mbalimbali
zitakazojitokeza.
Mradi wa ujenzi wa bomba hilo unagharimu dola za Kimarekani Bilioni Nne ambapo utaongeza ajira nyingi pamoja na kodi.
Amesema kuwa bomba hilo litajengwa
nchini kwa asilimia 90 kutokana na amani iliyopo ukilinganisha na
nyingine zilizo katika mradi huo.
Profesa Ntalikwa amesema kuwa kigezo
cha kwanza cha kujenga bomba nchini ni kutokana na Bandari ya Tanga kuwa
na kina kirefu cha kufanya kila meli kuweza kuingia hapo na tofauti
bandari ya Mombasa nchini Kenya.
Amesema kutokana na vigezo vinaashiria
kujengwa nchini licha ya kuwepo kwa majadiliano yanayoendelea juu ya
bomba hilo litajengwa wapi.
Amesema kuwa nchi ya Kenya ndio
inayofanya kuwa katika mchakato wa mwisho hivyo wenyewe ni watu wa
kuangalia tu jinsi ya mradi utapofanyika.
Aidha Profesa Ntalikwa amesema
kuwashirikisha wafanyabiashara wa mafuta ni kutaka kukujua fursa zilizo
katika ujenzi wa bomba la mafuta wa kuweza kuomba zabuni.
Chanzo, Glob ya Jamii
No comments:
Post a Comment