Tangakumekuchablog
Tanga, CHAMA Cha
Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), kimesema bajeti ndogo inawakwaza kuweza
kukabiliana na changamoto za kuwalinda watoto kupata haki zao.
Akizungumza katika kongamno la siku
moja la maofisa polisi, mahakimu na maofisa ustawi wa jamii jana, Mjumbe wa
baraza Tawla Makao Makuu, benadela Hassan, alisema ufinyu huo unashindwa
kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Alisema upungufu wa maofisa Ustawi
wa jamii ni chanzo cha haki za watoto na wanawake kupindishwa hivyo kuishauri
Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii na watoto na wazee kuongeza
maofisa ustawi wa jamii kila kata.
“Bajeti ndogo imekuwa kikwazo cha
Tawla kufanya kazi zake zikiwemo za kuhakikisha ulinzi wa watoto na wanawake
kupata haki zao, hatuna maofisa ustawi wa jamii wa kutosha” alisema Benadela
Alisema ili kuweza kuzilinda haki
hizo za watoto na wanawake ni Serikali kuhakikisha inaweka maofisa maendeleo
jamii ili kuweza kusimamia haki hizo tofauti na ilivyo sasa ambapo watoto
hawatendewi haki.
Kwa upande wake, Hakimu mkazi Mfawidhi
Wilaya Tanga, Azaiza Lutalla, alisema wazazi wanashindwa kuwachapa watoto wao
kwa hofu ya kupelekwa katika madawati ya jinsia.
Alisema kuna baadhi ya wazazi
wanawaogopa watoto kuwachapa hivyo kuyataka madawati kutoa elimu majumbani
namna ya kutoa adhabu kwa watoto wanapokosea.
“Kuna wazazi wanawaogopa kuwachapa
watoto kwa hofu ya kuwapeleka katika madawati ya kijinsia, je hapa inakaaje
kwani kwa hofu hiyo watoto hawataweza kuwa na maadili mema ya Kitanzania”
alisema Lutalla
Alisema ili kuweza kujua haki za
wazazi na watoto hasa wanawake ni wajibu wa madawati ya kijinsia kuhakikisha
inatoa elimu majumbani na kuweza kutokomeza unyanyasaji kwa wanawake na watoto
majumbani.
Mwisho
Wakili wa Serikali, Jeniffer Kaaya, akizungumza kwenye kongamano la Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (Tawla) lililofanyika jana Tanga na kuwashirikisha makundi mbalimbali pamoja na dawati la Jinsia na Watoto Tanga kupitia ofisi ya kamanda wa polisi Mkoa jana.
Picha ya pamoja viongozi wa Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (Tamla) baada ya kumalizika kongamano la siku moja kujadili Changamoto zinawakabili wanasheria nchi.
No comments:
Post a Comment