Tangakumekuchablog
Korogwe, MBUNGE
wa jimbo la Korogwe Vijijini (CCM), Stivin Ngonyani maarufu
Majimarefu,amewataka wananchi kujiandaa na mvua zinazotarajiwa kunyesha kwa
kutayarisha mashamba na kuacha kuuza kwa wageni.
Akizungumza katika mikutano ya
hadhara jana kata ya Kizera na Foroforo, Majmarefu aliwataka wananchi kuacha
kuuza mashamba na badala yake kujiandaa na mvua zinazotarajiwa kunyesha hivi
karibuni.
Alisema kuna taarifa za wageni
kuwarubuni wakulima kuuza mashamba yao kwa bei rahisi kwa kitisho cha mvua
kuacha kunyesha hivyo kuwambia kuwa waache kwani mvua zipo na karibuni
zitanyesha.
“Ndugu zangu wazee wangu na wajomba
zangu nimepata taarifa za kuwepo kwa watu kutoka nje ya hapa kuja kuwarubuni
ili muwauzie mashamba yenu, nawaomba chonde chonde musithubutu kwani mutakuja
jutia” alisema Majimarefu na kuongeza
“Wanakuja na pesa zao za uchwara kisha
kuwaingiza katika umasikini na njaa, mimi kama mbunge wenu sitakubali na
ninalifuatilia kwa ukaribu taarifa hizi kwani zimenisononesha” alisema
Akizungumzia upatikanaji wa pembejeo
za kilimo na uwepo wa maofisa ugani mashambani, Mbunge huyo alisema atahakikisha
Serikali inawapeleka maofisa hao na kuwa karibu na wakulima.
Alisema mara nyingi wakulima wanashindwa
kupata mavuno mazuri baada ya kukosa wataalamu wa kilimo hivyo msimu huu wa
kilimo atahakikisha maofisa hao wanakuwa karibu na wakulima.
“Kila mtu anajua kuwa maofisa kilimo
kwa baadhi ya maeneo hawafiki waliko wakulima, ndio maana hukosa mavuno na
balaa la njaa huwakumba” alisema
Aliwataka wakulima kutayarisha
mashamba yao na kujiandaa na kilimo kwa madai kuwa mvua ziko karibuni kunyesha
hivyo katika kufanikisha kilimo hicho ofisi yake ya mbunge itasaidia
upatikanaji wa mbegu.
Mlima mkubwa uliopo kata ya Kizara Korogwe Vijijini kama ilinavyoonekana
Moja ya majengo kata ya Kizara Korogwe Vijijini katika muonekano wake
Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Stivin Ngonyani, maarufu Majimarefu, akizungumza na wananchi kata ya Foroforo kwenye mkutano wa hadhara kuwashukuru kwa kumchagua kwa mara nyengine tena jana.
Wananchi kata ya Foroforo Korogwe Tanga, wakimsikiliza Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stivin Ngonyani, maarufu Majimarefu wakati wa mkutano wa hadhara kutoa shukurani kwa kumchagua tena kuwa Mbunge wao.
Vijana wa Kata ya Magoma Korogwe jimbo la Korogwe Vijijini wakipozi na Gari la Mbunge wao Prosefa Majimarefu jana wakati alipoenda kuwasalimu na kuwashukuru kwa kumchagua tena kuwa mbunge wao na kusikiliza kero zinazowakabili.
No comments:
Post a Comment