Thursday, March 10, 2016

SUMATRA WACHARUKA



Tangakumekuchablog
Tanga, AFISA Mfawidhi Sumatra Tanga, Walukani Luhamba, ametishia kuzizuia leseni za biashara za wasafirishaji abiria wa Mabasi ya Mikoani na Wilayani ikiwa hawatapunguza  nauli na kushikilia za zamani.
Akizungumza na vyombo vya habari mapema leo, Luhambo amesema Sumatra imetoa bei elekezi kufuatia soko la mafuta kuteremka bei hivyo kudai kuwa hakuna haja ya kung’ang’ania nauli za zamani.
Amesema soko la mafuta limekuwa likiteremka bei mfululizo na kudai kuwa wamiliki wa mabasi na magari ya abiria ya Wilayani wamekuwa waking’ang’ania bei za zamani hivyo kutoa agizo la kushuishwa kwa nauli mara moja.
Amesema kampuni yoyote ambayo itakaidi agizo hilo itashikilia leseni ya biashara na kuwapeleka mahakamani hivyo kuwataka kufanya marekebisho kabla ya ukaguzi kuanza.
Amesema Sumatra inatarajia kufanya ukaguzi katika vitua vya mabasi ya Mikoani na Wilayani na kuagiza nauli elekezi kufuatwa vyenginevyo mkondo wa sheria utafuta mkondo wake.
                                                    Mwisho

No comments:

Post a Comment