Thursday, March 31, 2016

BAADA YA MCC NA HAWA WENGINE WAMETANGAZA

Baada ya MCC, hawa ni wengine waliotangaza kusitisha misaada kwa Tanzania kisa uchaguzi wa Znz

March 29 2016 bodi ya shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilisitisha msaada wa awamu ya pili wa kutoa zaidi Trilioni 1.4 kwa Tanzania kutokana na kile lilichosema kuwa ni kufanyika kwa uchaguzi Zanzibar licha ya malalamiko ya uchaguzi huo lakini pia sheria mpya ya makosa ya mitandao Tanzania.
Sasa leo March 31 2016 shirika la utangazaji la Uingereza BBC kupitia bbcswahili.com limeandika ripoti ifuatayo >>>kundi la watoa misaada 10 kutoka nchi za magharibi limetangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania, hii inafuatia uamuzi wa shirika la utoaji misaada la serikali ya Marekani kuondoa msaada kutokana na uchaguzi wa Zanzibar ulivyoendeshwa
Karibu theluthi moja ya bajeti ya Tanzania ilitegemea msaada mwaka uliopita, kwa hivyo hatua hizo za hivi punde ni pigo kwa mipango ya maendeleo ya serikali mpya‘ – BBC SWAHILI.
Kwa habari matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment