Tarajia kuuona uwanja wa FC Barcelona katika muonekano huu 2021
Klabu ya FC Barcelona ya Hispania ambayo imezoeleka kutumia uwanja wake wa Nou Camp, March 9 imetoa picha za muonekano wa uwanja wao utakavyokuwa kwa miaka minne ijayo. FC Barcelona wametoa pichaz ramani ya ujenzi wa uwanja huo ambao utajengwa kwa thamani ya Pound milioni 465.
Mabingwa hao wa Ulaya wamethibitisha kuwa mchora ramani na mbunifu wa Kijapan Nikken Sekkei
ndio ameshimda tenda ya kufanya ukarabati wa uwanja huo hadi
utakapokamilika 2021, ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 105000.
No comments:
Post a Comment