Ndege ya Misri iliotekwa nyara yatua Cyprus
Ndege iliotekwa nyara imetua katika uwanja wa ndege wa Larnaca nchini Cyprus.
Duru za ndege hiyo pamoja na zile za serikali ya Misri zimenukuliwa
zikisema ndege hiyo ya abiria iliokuwa ikisafiri kutoka mjini Alexandria
kuelekea Cairo ilitekwa nyara na watu waliojihami.
Waliiamrisha ndege hiyo kutua Cyprus, msemaji wa shirika la ndege la AirMisri alinukuliwa akisema.
Shrika la habari la Cyprus limeripoti kwamba watu 55 wamo ndani ya ndege hiyo.
Kulikuwa na ripoti za awali kwamba zaidi ya watu 80 wamo ndani ya ndege hiyo.
Ndege hiyo aina ya MS181,airbus A320 ilibeba abiria 81.
Abiria aliyedaiwa kuwa alikuwa amevaa ukanda wa mlipuaji wa kujitolea
mhanga aliagiza rubani kuelekea Cyprus kulingana na AgyptAir.
Maafisa wa polisi wa Cyprus wamesema kuwa wale walioiteka hawakuitisha chochote ilipotua.
Uwanja wa ndege wa Larnaca umefungwa huku ndege zilizosubiriwa kutua zikielekezwa kwengineko.
No comments:
Post a Comment