Thursday, April 28, 2016

MACHIMBO YA KOKOTO NA MAWE AMBONI TANGA

 Wakazi wa Tanga wanadaiwa kutotembelea sehemu za historia na badala yake huwa wanahadithiwa vikiwemo vivutio vya Mapango ya Amboni, Mbuga ya Saadan na Beach yenye uwanda mkubwa wa pwani ya Raskazone ambazo zote zimekuwa zikipokea wageni kutoka ndani na nje ya nchi.
Kivutio cha Mapangio ya Amboni ni kilometa kumi tu kutoa mjini lakini wengi wao ukiwauliza hawajafika.
Hivi karibuni aliekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa aliwataka watu kuwa na ada ya kutembelea vivutio vya utalii na kufanya utalii wa ndani.
 Eno la Amboni ambalo linadaiwa kuwepo kwa shimo kubwa ambalo limefika hadi Mkoani Kilimanjaro na jengine Mombasa nchini Kenya  na kwa sasa kunafanyika uchimbaji wa mawe na kokoto.





Mkazi wa Amboni Tanga, Juma Maperege, akibanja mawe katika mgodi wa Amboni Tanga, wachimbani wa mawe na kokote kwenye mgodi huo wamekuwa wakilalamika kukosa soko na badala yake wamekuwa wakilanguliwa na madalali ambao huja na kuwalipata pesa ndogo na wao kuuza kwa bei kubwa kwa wateja mjini.


  Wajasiriamali wakazi wa Amboni Tanga, wakibanja mawe kisha kupata  kokoto katika mgodi wa Amboni. Wajasiriamali hao wamekuwa wakilalamika kukosa soko la uhakika la kuuzia kokoto zao na badala yake wamekuwa wakilanguliwa na madalali.



 Eneo la Amboni mashimbo ya Kokoto na Mawe Tanga
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment