Tangakumekuchablogspot.com
Tanga, KOCHA
Mkuu wa Coastal Union ya Tanga, Ali Jangalu, amesema ushindi walioupata wa bao
moja kwa Ruvu JKT, ni sawa na kuwapeleka
nusu fainali ya mashindano hivyo kila timu iliyoko mbele yao ni ushindi tu.
Jangalu alisema hayo mara baada ya
kuisha kwa mchezo wake na Ruvu JKT uwanja wa Mkwakwani jana, na kusema morali
wa ushindi waliupata wakati walipotoa kipigo kizito Simba wiki moja iliyopita.
Alisema wachezaji wake wameingiwa na
hamasa ya ushindi na wamekuwa wakicheza kwa kuelewana na kudhamiria kila mchezo
ulio mbele yao kupambana kupata ushindi
kuepuukana na janga la kushika daraja.
“Mchezo ulikuwa mgumu kwani
wapinzani wetu niseme ukweli walicheza vizuri zaidi ya sisi lakini nasi
tulipambana vya kutosha hadi dakika ya mwisho, ushindi huu ni sawa na kuingia
nusu fainali ya ligi hii ukifungwa mechi moja umekula mweleka” alisema Jangalu
na kuongeza
“Lakini pia ushindi huu umekuwa
mtamu zaidi kwa ndugu zetu African Sports pale tutakapokutana nao, nadhani
mechi hiyo ni sawa na fainali ya kombe la dunia” alisema
Jangalu alisema kwa ushindi huo mfululizo
wamedhamiria kupambana kufa na kupona na kuwambia wachezaji wake kuwa sasa
hakuna kuremba mipira bali na mashuti tu langoni mwa wapinzani toka dakika ya
kwanza hadi dakika za nyingeza za mwamuzi.
Kwa upande wake, Kocha wa Ruvu JKT,
Abdalla Kibadeni, alisema Coastal Uniona wako na bahati na kusema kuwa
wachezaji wake walicheza zaidi ya wao hivyo pointi tatu kuwaangukia wao.
Alisema walicheza zaidi ya wao
lakini uwanja uliokuwa na maji uliwasaidia kupata bao kwa kutumia uzoefu hivyo
na kusema kuwa safari bado ni ndefu na wanarudi kujipanga upya.
Alisema wachezaji wake walicheza
vizuri na hakuna hata mmoja alieonyesha
kucheza chini ya kiwango lakini bahati ya Mungu ikimuangukia mja hauwezi
kuipangua.
“Sisi tulicheza vizuri zaidi yao
lakini niseme kuwa bahati ya mja Mungu akimruzuku hakuna wa kuipangua na leo
hii ndio imetokea kwa Coastal, uzoefu wa uwanja uliokuwa na maji pia
umewasaidia” alisema Kibadeni
Alisema ligi ilipofikia bado wako na
nafasi ya kusonga mbele mbali ya upinzani mkubwa kwa timu ambazo zinafunga na
pointi na kusema kuwa watapambana hadi mchezo wa mwisho.
Mwisho
Washabiki wa Coastal Union ya Tanga,
wakiishangilia timu yao wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara na
Ruvu JKT Uwanja wa Mkwakwani jana,
Coastal Union ilishinda kwa bao 1.
Kocha wa Coastal Union ya Tanga, Ali Jangalu, akimuangalia mchezaji wake, Yussuf Chuma akichuana na mabeki wa Ruvu JKT, wakati wa mchezo ligi kuu Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani jana. Coastal Union ilishinda kwa bao 1.
Mchezaji wa Coastal Union, Chidebere Abdisalam, na mchezaji wa Ruvu JKT Renatus Morris, wakifukuzia mpira wakati wa mchezo ligi kuu Tanzania Bara uwanja wa Mkwakwani jana , Coastal Union ilishinda kwa bao 1.
No comments:
Post a Comment