Msimamo wa Ligi Kuu Ulivyo kwa sasa
Baada ya malalamiko ya muda mrefu kuhusu klabu ya Dar es Salaam Young Africans kuwa na viporo vingi, hatimae April 16 2016 wamemaliza michezo yao ya viporo kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Yanga walikuwa na michezo ya viporo mitatu na watani zao wa jadi Simba walikuwa wakilalamika Yanga kupendelewa kwa kwa mechi zake kusogezwa mbele, hivyo hawakuwa radhi kuendelea kucheza wakati wakihisi kuna dalili za upangaji wa matokeo.
Mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar hakuwa mwepesi kwa Yanga kwani Mtibwa walionekana kuwa na kikosi kizuri, kitu ambacho kilipelekea dakika 45 za kwanza kumalizika kwa kutofungana, mambo yalibadilika dakika 2 baada ya mchezo kuanza pale winga mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva alipoipatia Yanga goli la kuongoza na hatimae mchezo kumalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Uwanja wa Mkwakwani Tanga, Coastal Union waliutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kipenga cha mwisho dakika 90 kuibuka na ushindi mwembamba wa bao lililofungwa dakia ya 34 kipindi cha kwanza.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment