Friday, April 22, 2016

LICHA USHINDI MNONO JANA USIKU, WASHABIKI WACHARUKA


Yaliyoikuta Manchester United ilipokuwa ikicheza dhidi ya Crystal Palace yametokea kwenye uwanja wa Emirates usiku wa jana  wakati Arsenal Ikicheza dhidi ya West Brom ambapo uwanja mashabiki wengi wa Arsenal hawakujitokeza uwanjani kushuhudia mchezo huo kama ilivyo kawaida yao.

Takwimu zilizotolewa na maofisa wa timu hiyo zinasema kulikuwa na watazamaji wapatao 59,000 wakati uwanja wao unauwezo wa kubeba mashabiki 60,432 lakini takwimu za viongozi hao ni kwa mujibu wa tiketi zilizouzwa na siyo watu walioingia uwanjani kushuhudia mtanange huo.

Uamuzi wa mashabiki kutoingia uwanjani ni moja kati ya shinikizo la kutaka uongozi wa timu hiyo kumtimua Arsene Wenger katika kikosi cha The Gunners kutokana na kushindwa kutwaa taji la VPL kwa muda mrefu pamoja na kuishia kwenye hatua ya 16 bora mara sita mfululizo kwenye michuano ya mabingwa  Ulaya.

No comments:

Post a Comment