Aliyemtukana Rais Magufuli kwenye Facebook kapata dhamana
Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imempa dhamana Mtuhumiwa Isaac Abakuki anayetuhumiwa kumtukana Rais John Magufuli kupitia kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.
Hakimu mfawidhi Agustino
Rwezire amesema Mahakama baada ya kupitia hoja mbili zilizotolewa na
upande wa mashtaka na mshtakiwa, imeridhia kutoa dhamana kama haki ya
msingi ya mshtakiwa kutokana na kosa alilotenda ambapo dhamana hiyo ni
ya Wadhamini wawili waliotakiwa kuwa na jumla ya shilingi milioni tano.
Kwenye siku ya kwanza
kufikishwa Mahakamani Polisi walisema Tarehe 17 March 2016 Isaac Abakuki
akiwa nyumbani kwake Olasiti Arusha alipokea ujumbe kwenye account yake
ya Facebook ukisema ‘mnamlinganishaje Magufuli na Nyerere’ ukiwa ni
Ujumbe wa mjadala ulioanzishwa kwenye mtandao wa kijamii kufuatia hatua
ya Rais Magufuli kupiga simu kwenye kipindi cha Clouds 360 CloudsTV na kuwapongeza Watangazaji wa kipindi hicho.
Baada ya kusoma huo ujumbe Mtuhumiwa aliandika comment kujibu alichokisoma na kuandika >>> ‘Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi buana“…..
comment ya mtuhumiwa iliwaudhi na kuwakwaza watu wengi walioona
Facebook na wakaamua kufikisha malalamiko yao kwa mamlaka ya mawasiliano
Tanzania TCRA. – Polisi
TCRA kwa kushirikiana na
Polisi baada ya kufanya uchunguzi wa kina walifanikiwa kumkamata
Mtuhumiwa 22 March 2016 kwenye hoteli ya Annex Arusha na alipandishwa
Mahakamani kwa mara ya kwanza April 15 2016, kesi yake itaendelea tena
May 17 2016.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment