Baada ya Wenger kupata taarifa kuwa mashabiki wa Arsenal hawatokuja uwanjani leo April 21 2016
April 21 2016 hii inaweza ikawa siku ambayo kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger hatoisahau kama kweli itatokea kama ambavyo inaripotiwa na mitandao, kuwa mashabiki wa Arsenal wamepanga kutokwenda uwanjani leo April 21 2016 katika mchezo kati ya Arsenal dhidi ya West Brom ili kushinikiza Wenger aondoke.
Baada ya stori hizo kuenea mitandaoni waandishi wa habari walimpata kocha wa Arsenal Arsene Wenger azungumzie
kuhusu hiyo stori, kama mashabiki wakigoma kweli kuja uwanjani katika
mechi ya leo April 21 2016 ataendelekea kusalia Arsenal au ataondoka?
“Siwezi
kuzungumzia suala la mimi kuondoka Arsenal tena, bado na mkataba na
Arsenal na nina hueshimu, kuhusu mashabiki kutokuja uwanjani kila mmoja
ana maamuzi yake na tiketi yake ya msimu, mtazamo wa watu kupenda
kujaji, ni tabia ambayo tunalazimika kuishi nayo lakini ipo ndani ya
uwezo wetu kuibadili” >>> Wenger
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment