Wednesday, April 27, 2016

TAKWIMU ZA NCHI KUMI KUKUA KIUCHUMI KWA HARAKA IMETOLEWA

 list za nchi 10 zinazotajwa Uchumi wake utakua kwa haraka zaidi duniani, Tanzania ikiwemo

Ripoti ya World Economic Outlook ‘WEO’ ambayo inatoa makadirio ya maendeleo ya kiuchumi katika ngazi ya kimataifa, ripoti hiyo hutolewa April na September/October kila mwaka ambapo hutumia database kupata taarifa za akaunti za taifa, mfumuko wa bei, viwango vya ukosefu wa ajira, bei za bidhaa n.k.
Katika ripoti yake ya April 2016 imeitaja nchi ya Myanmar kuwa ndio nchi inayotajwa kuongoza nchi zinazotarajiwa kurejea katika ukuaji mkubwa wa uchumi kwa pato linalokadiriwa kukua kwa 8.6% kwa mwaka.
Ivory Coast imekuwa nchi ya pili na makadirio ya ukuaji wa pato la Taifa la 8.5% mwaka huu. Nchi zingine zilizotabiriwa kurudi takwimu ya juu ya ukuaji ni pamoja na India, Laos na Tanzania.
economic
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment