Tangakumekuchablog
Tanga, KOCHA wa
Coastal Union, Ali Jangalu, amesema anakubali mamuzi ya mwamuzi ya kupokea
kipigo cha mabao mawili kutoka kwa Yanga, lakini amedai hakuna ubishi timu yake
imehujumiwa.
Alisema hayo jana mara baada ya dakika
105 ya mchezo wake na Yanga uwanja wa
Mkwakwani, na kudai kuwa bao la Hamis Tambwe halikuwa sahihi na badala yake alikuwa
ameotoea.
Alisema timu yake ilicheza zaidi ya
Yanga lakini bahati haikuwa yao hivyo maamuzi ya mwamuzi ndio sahihi na hana la
kusema hivyo anawaachia washabiki walivyoliona goli la pili .
“Uzuri wa mchezo huu ulikuwa
unaonyeshwa moja kwa moja, mimi nikilalamika kama bao lile halikuwa sahihi
nitaonekana kama naminyana, kwa hivyo nawaachia wao waseme” alisema Jangalu na
kuongeza
“Hata kama tuko katika janga la
kushuka daraja lakini timu yangu ilicheza vizuri zaidi ya wao, niseme kuwa
hatuna bahati ya ushindi kila siku sie tunacheza vizuri lakini tunafungwa”
alisema
Alisema kama mwamuzi asingelivunja bambano
hilo mchezo ungelikuwa wao na kuwapongeza wachezaji wake kwa kuonyesha kandanda
safi ya kuvutia na kuwataka kusahau ya mwamuzi na kuangalia michezo iliyoko
mbele yao ligi kuu.
Alisema kila mchezaji alicheza kwa
kujituma na kujua wajibu wake uwanjani na kwa matokeo hayo anawapongeza na
kuongeza morali uwanjani ili michezo iliyoko mbele yao waweze kushinda.
Kwa upande wake mshambuliaji wa
Coastal , Ahmed Shiboli alisema Yanga waliwashika kila idara na kusema kuwa
walikuwa na bahati ambayo wanatakiwa kuishukuru kwani wangeondoka kwa aibu.
Alisema kwa mchezo walivyouanza toka
dakika ya kwanza ya mchezo ni dhahiri walipaswa kuondoka na pointi tatu ambapo walipeleka mashambulizi mengi langoni
mwao
Alisema beki ya Yanga waliisumbua na
baadhi ya mashuti kuokolewa na kipa wao ambao upande wa kiungo Abdulhalim
Humood aliisumbua safu ya ushambuliaji ya Yanga.
Mwisho
No comments:
Post a Comment