Wednesday, April 27, 2016

YANGA KICHEKO

Majibu ya mechi ya FA iliyovunjika Coastal Union vs Yanga imetolewa leo April 27

Kama ni shabiki wa soka la Bongo na ungependa kujua hatma ya matokeo ya mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA iliyochezwa Tanga katika uwanja wa Mkwakwani kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga na ilivunjika wakati Yanga wakiwa mbele kwa goli 2-1 hadi dakika 30 za nyongeza.
Uamuzi uliyofanywa na Kamati ya mashindano ya TFF jana  April 27 2016 wakizingatia kanuni ya 28(2) ya Kombe la shirikisho kuwa, Yanga inapewa nafasi ya kufuzu hatua ya fainali baada ya mchezo huo uliochezwa April 24 2016 kuvunjika Yanga wakiwa mbele kwa goli 2-1 na mashabiki wa Coastal Union ndio waliosababisha mchezo uvunjike.
Coastal Union kutokana na mashabiki wake kufanya vurugu katika mchezo huo wamepigwa faini ya Tsh 2000,000, wakati refa wa mchezo huo Abdallah Kambuzi amefungiwa mwaka mmoja na mwamuzi msaidizi namba mbili Charles Simon ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi hiyo ni kwa mujibu wa kanuni 38(1) ya Ligi Kuu.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment