Tangakumekuchablog
Tanga, WATOTO
wawili wakazi wa Kange Kasera Tanga , Antony Godfrey (3) na Emmanuel Aidan
(4) wamekufa maji baada ya kutumbukia
katika shomo la choo lililopo nje ya nymba ya jirani yao.
Tukio hilo limetokea jana saa 4
asubuhi na kuthibitishwa na kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Poul na kusema kuwa polisi inafanya uchunguzi wa
tukio hilo ili kama kulikuwa na uvunjaji wa sheria ya ujenzi sheria ziweze
kuchukuliwa.
Akizungumza tukio hilo baba mzazi wa
Antony, Godfrey Komba, alisema alipata taarifa za mtoto wake kufa maji akiwa
njiani akitokea kazini jambo ambalo lilimchanganya kwani asubuhi yake aliwaacha
wakiwa na afya njema.
Alisema alipatwa na mshtuko baada ya kupata taarifa za tukio hilo
na wakati alipokuwa akikaribia nyumbani kwake alimkuta mke wake, Flora Vicent
akilia na majirani wakiwa wamekusanyika kwa wingi.
“Hapa jirani kuna shimo la choo liko
mbele ya mlango wake na lilikuwa limejaa maji mengi na lilikuwa halijafunikwa,
watoto wangu na wajirani wamekuwa wakicheza na mara nyingi nilikuwa nikiwambia
wasicheze karibu na lile shimo” alisema komba na kuongeza
“Shimo hili limejaa maji kufuatia
mvua kubwa ilionyesha juzi kwa siku mbili mfululizo, tukio limeshatokea sina la
kusema na kwa sasa ndio tunashughulikia mazishi” alisema
Wakizungumza na mwandishi wa habari
hizi kwa nyakati tofauti msibani hapo, wakzi wengi wameitaka mipango miji
kuweka sheria ya ujenzi hasa wa mashimo ya choo.
Walisema kuna baadhi ya wajenzi
wamekuwa wakichimba mashimo ya vyoo kisha kuyatekeleza na kuwa hatari kwa
watoto na mifugo.
Mwisho
Wakazi wa Kange Kasera Tanga, wakimfariji Flora Vicent, mama wa mtoto , Antony Godfrey Komba, aliekufa baada ya kutumbukia katika shimo la choo lililokuwa limejaa maji karibu na nyumba yao jana.
No comments:
Post a Comment