Friday, April 22, 2016

OBAMA AIANGUKIA UINGEREZA


 Rais Barack Obama amesema anaunga mkono Uingereza kubaki katika jumuiya ya Umoja wa Ulaya ili kuweza kuchangia katika vita dhidi ya ugaidi na masuala wahamiaji na utatuzi wa migogoro ya kiuchumi.

Rais Obama ameyasema hayo anapoanza ziara yake nchini Uingereza.

Rais Obama amenukuliwa na gazeti la Uingereza Telegraph, akisema kwamba uanachama wa Uingereza katika umoja wa Ulaya una umuhimu mkubwa na endapo nchi hiyo itajiondoa katika umoja huo itapunguza nguvu katika vita dhidi ya ugaidi duniani, suala la wahamiaji na utatuzi wa matatizo ya kiuchumi.

Uingereza kuamua kuhusu EU

Hata hivyo Obama amesema anatete hoja ya umoja wa Ulaya kuendelea kama ulivyo badala ya Uingereza kujitioa,japo kuwa anakabiliwa na upinzani kutoka kwa viongozi wa juu wa Uingereza wanapiga kampeni kujitoa katika umoja huo.

Johnson amesema Obama ameonyesha unafiki

Naye meya wa mji wa London Boris Johnson amesema Marekani isingeweza kuuza sehemu ya demokrasia yake kama ambavyo Uingereza imefanya kwa umoja wa Ulaya.

Hii leo Rais Obama anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon kwa mazungumzo na baadaye chakula cha mchana na malkia Elizabeth wa Uingereza hii ikiwa ni siku moja baada ya maadhimisho ya miaka 90 ya kuzaliwa kwake.

No comments:

Post a Comment