Kitilya na wenzake walifikishwa tena Mahakamani leo April 29 2016
Aliyekuwa Kamishna wa TRA, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi wa benki ya Stanibic tawi la Tanzania pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare April 27 2016 walikosa dhamana kutokana na upande wa Jamhuri kukata rufaa mahakama kuu kupinga maamuzi ya kupewa dhamana.
Leo April
29 2016 kesi hiyo ilitajwa kusikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es salaam ambapo awali Hakimu Mchauru alitoa maamuzi ya
kuahirishwa kwa kesi hiyo mpaka Mei 12 mwaka huu, sababu ni kutokana na
jalada halisi la kesi kupelekwa mahakama kuu baada ya kukatwa kwa rufaa
ya kufutiwa shitaka namba nane la utakatishaji fedha.
Muda mfupi
baadae majira ya saa 4;30 asubuhi walirudishwa tena mbele ya Hakimu
Mchauru baada ya kupata amri kutoka kwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda
ya Dar es salaam akitamka kesi hiyo itajwe Mei 3 mwaka huu badala ya
mei 12, aliyoipanga awali.
Hakimu
Mchauru amesema sababu za kupewa amri hiyo hazijui, hivyo kesi itatajwa
tena Mei 3 mwaka huu na yale yaliyozungumzwa asubuhi yatabaki kama
ilivyo, watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment