Tangakumekuchablog
Tanga,
MSHAMBULIAJI wa Coastal Union ya Tanga, Ahmed Shiboli, ameiambia Yanga kuwa
wasitarajie kuchukua pointi tatu Tanga, bali watarajie kipigo kama walichokitoa
kwa Simba wiki mbili zilizopita.
Akizungumza mara baada ya kufanya
mazoezi Uwanja wa Mkwakwani leo, Shiboli alisema timu hiyo imeiva na iko
tayari kwa mchezo huo ambao watapigana kufa na kupona ili pointi tatu zibaki
Tanga.
Alisema kwa sasa timu hiyo iko kwa
kusubiri mchezo huo kwani wameibva na hakuna mapungufu kuanzia mlinda mlango
washambuliaji na kumezingatia mbinu walizopewa na wakufunzi wao.
“Kwanza mimi mwenyewe nakuhakikishia
nitafunga goli, kuna jambo nimeongeza wakati wa
mazoezi, ningekuwambia lakini sitakui kiwe hadharani kwani mabeki wa
Yanga wataniandama wakati wa mechi” alisema Shiboli na kuongeza
“Tunmekuwa tukifanya mazoezi kwa
siku mara mbili mfululizo na tumekuwa kambini na muda mwingi tumekuwa tukipewa
mbinu za kuimaliza Yanga, nikuhakikishie hatoki mtu kesho” alisema
Alisema anatambua kuwa Yanga itakuwa
ikicheza kama Mbogo aliejeruhiwa kwa kipigo cha Tunisia ila kwetu itakuwa
ikitupa morali kwani tukiweza kumfunga goli la mapema atanyongea.
Kwa upande wake Msemaji wa Coastal
Union, Osker Assenga, ameiambia Mwanaspoti kuwa wachezaji wameiva na wako
tayari kwa mpambano huo ambao alidai ushindi ni lazima.
Alisema hakuna sababu ya kupoteza
mchezo huo ambao ni muhimu na utakuwa umewajenga katika kinyang’anyiro cha
kubaki ligi kuu msimu ujao wa ligi ambapo amesema ligi iko lala salama.
“Niseme kuwa wachezaji wameiva na
wanasubiri siku ya kesho kuingia uwanjani, hatuna majeruhi wala mgonjwa,
tunwaomba wakazi wa Tanga kuja kuishangilia timu hiyo na kuibuka na ushindi”
alisema Assenga
Ameiambia Yanga kuwa wasitarajie
kuibuka na ushindi Mkwakwani kesho kwani watatoa kipigo kama ilichokitoa kwa
Simba wiki mbilizi zilizopita kwa kutumia uzoefu kwa uwanja na nyumbani.
Mwisho
No comments:
Post a Comment