Wahamiaji 400 kutoka Somalia wazama baharini
Maelfu ya wahamiaji kutoka Afrika na Mashariki ya Kati wamekuwa wakijaribu kufika UlayaWahamiaji karibu 400, wengi wao kutoka Somalia, wanahofiwa kuzama katika bahari ya Mediterranean wakijaribu kuelekea bara Ulaya.
Taarifa kutoka Misri zinasema wahamiaji hao walikuwa wakitumia boti nne kusafiri.
Jamaa za baadhi ya wahamiaji hao wamesema baadhi ya wahamiaji waliokolewa na kikosi cha wana maji kutoka Ugiriki na kupelekwa katika jiji la Grees..
Balozi wa Somalia nchini Misri amethibitisha kisa hicho lakini akasema bado wanatafuta maelezo zaidi kujua chanzo hicho na eneo la safari walioanzia.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment