HADITHI na Faki A Faki, 0655 340572 au 0713 340572
MWANAMKE ALIYENICHUNUKA 16 inaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu cha Candle Education Centre Tanga, Candle ni mabingwa wa kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu, Candle wapo na Hosteli na gari maalumu la kuwapeleka watoto shule, Candle wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746
ILIPOISHIA
Msichana huyo alitoa kichwa kwenye dirisha la gari na kuniambia.
“Kijana hujambo?”
“Sijambo. Habari yako?”
“Nzuri. Unarudi nyumbani?”
“Ndiyo,ninarudi nyumbani”
“Ingia garini nikupeleke. Nina mazungumzo na wewe!”
“Una mazungumzo na mimi?” nilimuuliza kama
vile sikumsikia vizuri.
“Mbona umeshituka?”
“Hapana, sikushituka”
“Basi ingia garini”
Nikafungua mlango wa upande wa pili wa dereva na kujipakia. Msichana
akalindoa gari.
SASA ENDELEA
“Unaitwa nani?” akaniuliza.
“Naitwa Alfred”
“Umeanza hizi kazi za ulinzi lini?”
“Nina muda mrefu isipokuwa kwenye kampuni hii niliyoko sasa, nimeanza
siku chache tu zilizopita”
“Sawa. Una mke na watoto?”
“Hapana, sijaoa bado”
Msichana aliniangalia akatabasamu kabla ya kuniuliza.
“Una mchumba?”
Na mimi nikatabasamu na kutikisa kichwa.
“Sina mchumba” nikamjibu.
“Unangoja nini?”
“Najiweka sawa kwanza”
“Unalipwa mshahara wa kiasi gani kazini kwako?” Msichana akaniuliza
baada ya kimya kifupi.
“Mshahara mdogo tu… haufiki hata laki moja”
“Nimekuuliza hivyo kwa maana. Ninahitaji mlinzi kwenye nyumba yangu.
Nimeona wewe unafaa. Nitakulipa mshahara mzuri”
Niliukumbuka sana
wema wa yule msichana, nikamuuliza.
“Nyumba yako iko wapi?”
“Iko Raskazoni”
Eneo alilolitaja lilikuwa linaishi watu wenye vipato vya juu.
“Unahitaji kulindiwa nyumba yako wakati wa mchana au usiku?”
“Kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi asubuhi”
“Sawa”
“Uko tayari?”
“Utakuwa unatoa likizo na siku za mapumziko?”
“Nitazingatia sheria zote za kikazi. Kwa wiki kutakuwa na siku moja ya
mapumziko zikiwemo siku za sikukuu na likizo ya mwaka. Pia ukiwa mgonjwa,
nitagharamia mimi matibabu yako”
“Sawa. Utanilipa mshahara wa kiasi gani?”
“Nitakulipa mshahara mzuri. Utaniambia wewe unataka nikulipe mshahara wa
kiasi gani kwa sababu ninakuhamisha kutoka mahali pengine”
“Ni vyema uniambie wewe, utanilipa kiasi gani?”
“Ingawa hukuniweka wazi kuhusu mshahara wako wa sasa, mimi nitakulipa
mara tatu ya mshahara unaopata”
“Sawa.”
“Je uko tayari?”
“Niko tayari. Unanihitaji kwa lini?”
“Hata kwa kesho”
“Kwa kesho haitawezekana. Subiri nimalize mwezi huu nipate mshahara
wangu”
“Samehe huo mshahara. Nitakulipa mimi. Kesho nitakupa shilingi laki
moja uandike barua ya kuacha kazi. Keshokutwa uanze kwangu”
“Kama ni hivyo sawa. Ukinipa laki moja
nitaandika barua ya kuacha kazi na kesho kutwa ninaanza kwako”
“Barua iandike leo, kesho unakwenda nayo”
“Na hiyo laki moja…?”
“Pia naweza kukupa leo. Lakini itabidi twende nyumbani kwangu, uione
hiyo nyumba na pia nikupatie hizo pesa”
“Sawa, twende tu”
Msichana akaligeuza gari na kuweka gea ya nyuma na kuelekea upande wa Raskazoni.
“Unaonaje maisha?” akaniuliza baada ya kimya kifupi.
“Tunaendeshana nayo hivyo hivyo”
“Lakini wewe huna mke wala watoto, una nafuu si kama
wengineo”
“Hakuna nafuu yoyote, maisha ni magumu dadangu”
“Kwa mshahara nitakaokupa, natumaini maisha utayamudu vizuri”
“Sisi binaadamu kila upatavyo zaidi ndivyo mahitaji yanavyoongezeka
zaidi”
Nilikuwa kiti cha mbele mara akaweka gea ya tatu huku akiniangalia kwa jicho la mahaba ila moyo wangu nao ukawa na fadhaa.
“Ni kweli Alfred, lakini unakuwa umepiga hatua ya kimaisha kuliko
ulivyo sasa”
Tulifika nyumbani kwake Raskazoni. Niliiona nyumba yake iliyokuwa kando
ya bahari. Lilikuwa jumba la kifahari la horofa moja tena lilikuwa jipya.
“Ndiyo hii nyumba yako?” nikamuuliza huku nikidhihirisha wazi mshangao.
“Ndiyo hii, ngoja tuingie ndani”
Geti la nyumba lilifunguka lenyewe kutokana na rimot iliyokuwa mbele ya
gari. Msichana akaliingiza gari ndani. Gari hilo
lilipoingia geti hilo
likajifunga tena.
Msichana huyo alisimamisha gari hilo
mbele ya mlango wa nyumba.
“Tushuke!” akaniambia huku akifungua mlango na kuitoa ile funguo ya gari na kushuka.
Na mimi nikashuka.
Msichana alitoa funguo na kufungua mlango wa nyumba.
“Karibu ndani Alfred” akaniambia huku akitangulia kuingia ndani na mimi
nikamfuata nyuma.
Ni vyema nikiri kuwa katika maisha yangu tangu nizaliwe sijawahi kuingia
ndani ya jumba zuri kama lile.
Nilijikuta nimeganda pale kwenye mlango nikiangalia humo ndani jinsi
mlivyokuwa mnapendeza na kujaa vyombo vya thamani. Niliona kama vile nikiingia,
viatu vyangu vitachafua.
“Mbona umesita kwenye malango?” Msichana akaniuliza alipoona nimesimama
kwenye mlango.
ITAENDELEA KESHO, ungana nami hapa hapa Tangakumekuchablog
|
Sunday, April 17, 2016
HADITHI MWANAMKE ALIENICHUNUKU SEHEMU YA (16)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment