Klabu imeamua kusitisha mkataba na staa wa zamani wa Arsenal kwa mambo mawili tu
April 25 2016 headlines zilizopo katika mitandao ya soka Uingereza na Ujerumani ni kuhusiana na mshambuliaji wa kimataifa wa Denmark aliyewahi kuichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza Nicklas Bendtner kuvunjiwa mkataba wake na klabu yake ya sasa ya Wolfsburg.
Nicklas Bendtner amevunjiwa mkataba na Wolfsburg baada ya uongozi wa klabu hiyo kutoridhishwa na mwenendo wa kinidhamu wa mchezaji huyo, Wolfsburg wamevunja mkataba na Nicklas Bendtner ambaye mkurugenzi wa michezo klabu hiyo Klaus Allofs alinukuliwa akisema Nicklas Bendtner ni hatari kwa klabu mkataba wake umesitishwa.
“Mshambuliaji Nicklas
Bendtner sio tena mchezaji wa Vfl Wolfsburg, mkataba wetu na mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye mkataba wake ulikuwa unaisha June
2017 umesitishwa rasmi na klabu kutokana na kulalakupitiliza na kwenda
katika timu akiwa kachelewa”
Bendtner aliondoka Arsenal 2014 baada ya kucheza kwa mkopo katika vilabu kadhaa na baadae akajiunga Wolfsburg kwa mkataba wa miaka mitatu, Bendtner hajaichezea timu yake ya taifa wala klabu toka February 6, lakini Wolfsburg walitangaza kumfungia mwezi March kabla ya leo April 25 2016 kutangaza kuvunja nae mkatabaKwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment