Wednesday, April 20, 2016

MCC KUJITOA UFADHILI HAKUTAKUWA NA ATHARI


Serikali imesema kujitoa kwa wafadhili wa Shirika la Changamoto za Milenia(MCC),katika miradi ya kuzalisha umeme hukujaathri utekeezaji wa miradi  ya usambazaji wa umeme vijijini.

Akitoa kauli hiyo ya Serikali jana Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani, amesema miradi yote ya shirika hilo ya awamu ya kwanza ilitekelezwa vizuri na kukamilika.

Dkt. Kelemani amesema kuwa katika utekelezaji wa miradi hiyo awamu ya pili serikali itatoa shilingi bilioni moja na kiasi kingine kitatolewa na benki ya Maendeleo ya Afrika AFDB na Benki ya dunia (WB).

Dkt. Kilimani amesema tayari Bank ya Maendeleo ya Afrika imesema itatoa shilingi bilioni moja Dola za Marekani na vilevile Benki ya dunia itatoa shilingi bilioni 3 dola Marekani ili kukamilisha mradio huo kwa awamu ya tatu kwa hiyo mradi huo hautatetereka.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment