Friday, April 29, 2016

MSEMAJI WA COASTAL UNION AJIPA MOYO



Tangakumekuchablog
Tanga, MSEMAJI wa Coastal Union ya Tanga, Oscar Assenga, amesemamechi ya leo  na ndugu zao African Sports ni sawa na fainal na atakaefungwa ajitambue kuwa ameshuka daraja.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Assenga alisema timu yake imejiandaa vya kutosha na iko tayari kwa mpambano huo ambao anatarajia kuwa mkali na ushindani wa hali ya juu.
Alisema ana imani kuwa African Sports nao wamejiandaa vya kutosha hivyo kuongeza ladha ya mashambulizi ya nguvu hivyo kuwambia ndugu zao kuwa wasitarajie kuondoka na pointi tatu uwanjani leo
“Nashani kila mtu anaona Coastal ilivyobadilidika toka iifunge Simba na kutoa upinzani mkali kwa Yanga, yuko vizuri na tuko tayari kwa mpambano huo na niseme kuwa pointi tatu muhimu ni za kwetu” alisema Assenga na kuongeza’
“Jambo ambalo linanipa matumaini ya kuibuka na ushindi ni kuwa hatuna majeuhi kikosi ni kile kile na kimejipanga vya kutosha na African Sports tutaifunga zaidi ya magoli mawili” alisema
Aliwataka washabiki wa timu hiyo kufika kwa wingi uwanjani na kuishangilia kwa nguvu ili timu yao kuibuka na ushindi na kupata pointi tatu muhimu ambazo zitawaweka katika matumaini ya kubaki ligi kuu msimu ujao.
Kwa upande wake  mshambuliaji, Juma Mahadhi, amesema kesho ataifunga Sports kwa madai kuwa katika michezo yake iliyocheza ameona mapungufu ya beki yake hivyo anajua namna ya kuipenya.
Alisema kama hatafunga magoli mawili basi japo atafunga hivyo kutarajia kpigo kutoka kwao ambacho amesema wachezaji wa Coastal wamejipanga vya kutosha na kuiva.
“Niwaambie kuwa mimi Leo  niftaunga magoli mawili na kama sio hayo basi japo moja, mchezo huu nimeupania vya kutosha kwani nimeiva na niko tayari kuwavaa” alisema Mhadhi
Aliwataka mabeki wa African Sports kuwa makini nae kwani mbinu za kocha wao, Ali Jangalu, zitawafanya kuibuka na ushindi mnono.
                                                  Mwisho

No comments:

Post a Comment