STARS KUJIPIMA NA HARAMBEE STARS MEI 29
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa
Stars) inatarajiwa
kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa Kenya (Harambee
Stars) Mei 29, 2016 jijini Nairobi.
Mchezo huo wa kirafiki utachezwa
jijini Nairobi Mei, 29 mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa timu
zote mbili kujaindaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa Fainali za
Mataifa Afrika mapema mwezi Juni, 2016.
TFF kwa kushirkiana na FKF
zimekubaliana kuwepo kwa mchezo huo wa kirafiki, utakotumika kama sehemu
za maandalizi kwa timu zote kujiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa
AFCON 2017 mwezi Juni.
Kikosi cha Taifa Stars
kianchonolewa na kocha mkuu, Charles Boniface Mkwasa kinatarajiwa
kuingia kambini mwezi Mei, mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya
Vodacom (VPL) kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki kabla ya kuwakabili
Misri katika uwanja wa Taifa jijini Dra es salaam Juni 04, 2016.
Stars inajianda na mchezo wa
kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika mwaka 2017 nchini Gabon
dhdi ya Misri utakaochezwa Juni 04, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment