Tangakumekuchablog
Tanga, KATIBU
Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma, Lauren Ndumbaro, amewataka madaktari na
wauguzi hospitali ya Rufaa ya Bombo Tanga, kufuata maadili ya kazi ikiwa na
pamoja na kutunza siri za wagonjwa.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi
kifaa maalumu cha matangazo cha kutolea taarifa za Afya kwa wagonja na
wafanyakazi hospitalini hapo kilichotolewa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani
(GIZ) juzi, Ndumbaro alisema kuna baadhi ya watumishi hukiuka maadili ya kazi
zao.
Alisema kuna tabia iliyojengeka kwa
wadaktari na wauguzi kutoa siri za wagonjwa na kusahau maalidili ya kazi hivyo kutaka
kuachwa tabia hiyo ambayo imekuwa ikiwadhalilisha wagonjwa katika jamii.
“Leo nimekuja hapa katika uzinduzi
wa kifaa cha matangazo kwa wagonjwa na wafanyakazi hospitali kilichotolewa
kupitia mradi wa ndugu zetu wa Ujerumani, kupitia hadhara hii niwatake
kuzingatia maadili ya kazi zenu” alisema Ndumbaro na kuongeza
“Kuna baadhi ya wauguzi na madakari
hutoa siri z wagonjwa jambo ambalo ni kinyume na maadili ya utumishi, ili
kuikomesha tabia hii kila mmoja awe askari wa mwenzake kupitia kitengo hiki cha
kupokea matangazo” alisema
Aliwataka watumishi hao kufanya kazi
kwa bidii na kuondosha malalamiko kwa wananchi juu ya huduma zitolewazo katika
hospitali na vituo vya afya vya Serkali nchini.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) Godwin Kabalika, amesema shirika hilo
limekuwa likisaidia hospitali mbalimbali kuboresha mifumo yake ikiwemo ya
mawasiliano pampja na utunzaji wa kumbukumbu za fedha.
Alisema mfumo huo wa mawasiliano kwa
wagonjwa na wafanyakazi utakuwa ukitoa taarifa mbalimbali za afya na
upatikanaji wa huduma sehemu husika ikiwa na pamoja upokeaji wa malalamiko kwa
wateja.
“Msaada huu ni moja ya miradi ya
shirika la Ujerumani katika kusaidia hospitali hapa nchini kuboresha mifumo
yake ya utunzaji kumbukumbu na mawasiliano na shughuli nyengine za kijamii
katika hospitali” aliksema Kabalika
Aliwataka wahusika wa kifaa hicho
cha mawasiliano kukitunza na kuwa msaada kwa wafanyakazi na wagonjwa kwa
kupeana taarifa pamoja na upokeaji wa taarifa za malalamiko na nyenginezo
zihusianazo na Afya.
Mwisho
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi
wa Umma, Dr, Laurent Ndumbaro (katikati)
akipatiwa maelezo na mganga Mfawidhi hospitali ya Rufaa ya Bombo, Dr,
Jumanne Karia (kulia) wakati alipotembelea mara baada ya kukabidhi kifaa cha
kutolea taarifa za wagonjwa na wafanyakazi hospitali (Paplic Adress System)
kupitia Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kushoto ni, Mkurugenzi wa Ukuzaji Maadili
Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma, Mathew Kirama.
Dakatari bingwa wa watoto hospitali ya Rufaa ya Bombo, Dr, Murtaza Rasheed (kulia) , akimpatia maelezo juu ya magonjwa ya watoto wakati alipotembelea hospitali hapo mara baada ya makabidhiano ya kifaa maalumu cha kutolea taarifa za wagonjwa na wafanyakazi kupitia mradi wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) jana.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma, Dr, Laurent Ndumbaro (kulia) akimkabidhi Katibu Tawala Msaidizi na Rasilimali watu, Bernard Messelini, kifaa maalumu cha kutolea matangazo kwa wagonjwa na wafanyakazi kupitia Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) makabidhiano yaliyofanyika jana.
No comments:
Post a Comment