Monday, April 25, 2016

ST CHRISTINA YAFUNIKA MAHAFALI TANGA



Tangakumekuchablog
Tanga, WAZAZI na Walezi Tanga wametakiwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni na kupiga vita michezo mitaani  wakati wa masomo lengo likiwa nikuondosha wimbi la watoto mitaani.
Akizungumza wakati wa mahafali ya 14 shule ya ST, Christina Girls Secondary School ya Tanga juzi, Afisa Elimu Mkoa, Mayasa Hashimu, alisema kuna wimbi kubwa la watoto  ambao wako na umri wa kwenda shule wanashinda mitaani.
Aliwataka kuhakikisha kila mzazi na walezi watoto wao wanashiriki kikamilifu masomo darasani na kupiga vita mchezo wa pool wakati wa kazi masomo  lengo likiwa nikuwajenga kielimu na kuwa msaada maishani mwao ya baadae.
“Hapa tupo wazazi walezi pamoja rika mbalimbali, kupitia hadhara hii ya kuwaaga watoto wetu, tuhakikishe kila mmoja anakuwa na wajibu wa kutambua kijana wake anaenda shule” alisema Mayasa na kuongeza
“Ofisi yangu niko na utaratibu wa kufanya ziara shuleni kuona mahudhuria ya wanafunzi darasani, sitakuwa tayari kuona idadi ya wanafunzi wa darasani inapungua na niko tayari kwenda hadi kwa mzazi” alisema
Alisema ili kulifanikisha lengo la mtoto kupata haki yake ya kupata elimu ni wajibu wa wazazi kuhakikisha wanashiriki masomo kikamilifu na kuacha kuwatumikisha kazi ambazo hawastahili kuzifanya.
Kwa upande wake, Afisa Taaluma Taasisi ya Counfusion Chuo Kikuu Dar es Salaam, Isaac Mbata, alisema kwa mara ya kwanza wataanza kufundisha lugha ya Kichina katiba baadhi ya shule nchini na kuanzia wataanza na ST Christina ya Tanga.
Alisema uamuzi wa kufundisha lugha hiyo ni kuona umuhimu mfumo wa utandawazi katika biashara  na kupendelea kuanza shule ya ST Christina na nyengine kutajwa mbeleni.
“Umuhimu wa kufundisha kichina kwa baadhi ya shule ni uamuzi tuliooa utakuwa sahihi kwanza kibishara na mahusiano ya wenzeti ambao tumekuwa tukienda kwao mara kwa mara na wao pia wapo wengi hapa nchini” alisema Mbata
Mbata aliwataka wanafunzi hao kulipokea wazo hilo la lugha ya kichina ambalo amesema mbali ya kujua lakini pia ni moja ya sehemu ya lugha za kigeni ambayo inaweza kumpatia mtu ajira mbele ya safari katika maisha.
                                                Mwisho


 Wanafunzi wa kidato cha sita shule ya Srkondari ya ST Christina ya Tanga, wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kutunukiwa vyeti wakati wa mahafali ya 14 shuleni hapo juzi. Jumla ya wanafunzi 121 walimaliza masomo yao.




Wahitimu wa kidato cha sita shule ya Sekondari ya ST, Christina  Tanga, wakiingia ukumbini wakati wa mahafali ya 14 shuleni hapo juzi, Jumla ya wahitimu 121 walimaliza masomo ya kidato cha sita juzi.

No comments:

Post a Comment