Tuesday, April 19, 2016

COASTAL UNION ILIYOIVA IKO TAYARI KUTOA KIPIGO KWA YANGA FA JUMAPILI



Wachezaji wa Coastal Union ya Tanga wakifanya mazoezi uwanja wa shule ya Msingi ya Bombo kujiandaa na mchezo wake wa nusu Fainali (FA) na Yanga uwanja wa Mkwakwani Jumapili.
Coastal imepania tena kuzidunda timu za Simba na Yanga katika uwanja wake wa Mkwakwani na kudai kuwa ushindi Jumapili ni wa lazima na hakuna cha kupoteza.
Wamedai kuwa kwa sasa wamepata mbinu nyenguine mpya ya kuidunda Yanga baada ya mazoezi makali wanayopatiwa na wakufunzi wao pamoja na mbinu za uwanjani kwa kocha wao Ali Jangalu.
Wachezaji hao wamedai wamekuwa wakifanya mazoezi mfululizo asubuhi na jioni na wako tayari kwa mchezo huo na kusema kuwa wameupania ili kutoa salamu kwa timu za ligi kuu zilizosalia ambazo wameadhimia kutoa kipigo kila timu itakayokutana nayo.








No comments:

Post a Comment