Tuesday, April 19, 2016

AZAM FC YATUMBULIWA MAJIPU TUSISIA

Azam FC wameshindwa kuendelea na michuano ya CAF, baada ya kipigo hiki …


April 19 2016 wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Africa (CAF) klabu ya Azam FC ilishuka mjini Rades Tunisia kucheza mchezo wake wa marudiano wa Kombe la shirikishoa barani Afrika dhidi ya klabu ya  Esperance ya Tunisia.
Azam FC ambao mchezo wa awali uliochezwa Chamazi Dar es Salaam waliibuka na ushindi wa goli 2-1, wamekubali kipigo cha goli 3-0 katika mchezo huo wa marudiano. Kabla ya mchezo huo Azam FC walikuwa wakihitaji ushindi au sare yoyote ya magoli ili waweze kusonga mbele. Magoli ya Esperance yalifungwa na Bguir, Jouini na Errouge.

Baada ya kuondolewa katika michuano kwa klabu ya Azam FC, Tanzania inabakia na muwakilishi mmoja pekee katika michuano ya kimataifa, ambaye ni klabu ya Dar esa Salaam Young Africans ambayo April 20 itacheza mchezo wake wa marudiano na wenyeji wake Al Ahly.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment