NEWS: Maamuzi ya Rais Magufuli kwa Mkurugenzi mwingine leo April 28 2016
Taarifa ambayo imetoka April 28 2016 ni kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji ‘TIC’, Julieth Kairuki kuanzia April 24 2016.
Hatua hii imechukuliwa baada ya Rais Magufuli
kupata taarifa kwamba Mkurugenzi huyo hajachukua mshahara wa Serikali
tangu alipoajiriwa mwezi April 2013 mpaka sasa, jambo ambalo linazua
maswali mengi.
Taarifa
hiyo iliyotolewa imesema endapo atakuwa tayari kufanya kazi na Serikali
atapangiwa kazi nyingine na Clifford Katondo Tandari atakaimu nafasi ya
Mkurugenzi Mtendaji.
CHANZO, millardayo
No comments:
Post a Comment