Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Usagara Tanga wakifanya
usafi wa mazingira hospitali ya Bombo Tanga ikiwa ni kuunga mkono agizo la Rais
John Pombe Magufuli la kufanya usafi siku ya Jumamosi.
Wanafunzi hao wakiongozwa na Mwalimu wa Nidhamu wa shule hiyo, Bakari Kivuna na Kaka Mkuu wa wanafunzi, Geogre Gidion, walifanya usafi katika maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.
Akizungumza mara baada ya kumaliza ufanyaji usafi, Mwalimu huyo wa Nidhamu, alisema shule yake imekuwa na ada ya kufanya usafi katika maeneo yanayoizunguka jamii ikiwemo vituo Hospitali, Vituo vya Afya masokoni na maeneo mengine lengo likiwa ni kutekeleza agizo la Rais la kufanya usafi ili kutokomeza magonjwa ya miripuko ikiwemo Kipindupindu na magonjwa ya Kuhara.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Usagara Tanga wakipiga picha ya pamoja na walimu wao mara baada ya kumaliza kufanya usafi hospitali ya Bombo leo
No comments:
Post a Comment