Yahya Jammeh ameondoka Gambia na kuelekea Guinea
Yahya Jammeh,
aliyekuwa rais wa Gambia, ameondoka nchini humo na kuelekea nchini
Guinea baada ya kukubali kukabidhi madaraka kwa Adama Barrow
aliyemshinda katika uchaguzi wa urais mwezi disemba mwaka jana.
Jammeh alisafiri kwa ndege kutoka Banjul hadi Guinea na baadaye kuendelea na safari yake kwenda Equatorial Guinea.Hapo jana Jammeh alitangaza kwamba atang'atuka baada kuongozi Gambia kwa miaka 22.
Kwa mujibu wa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika magharibi ECOWAS, Jammeh amewasili nchini Guinea . Siku ya Alhamisi ECOWAS illituma vikosi vyake nchini Gambia kumshurutisha Jammeh kukubali Adama Barrow aapishwe.
Jumuiya hiyo inasema imesitisha oparesheni yake ya kijeshi Gambia lakini wanajeshi elfu saba watasalia nchini humo kudumisha usalama, huku Adama Barrow akitarajiwa kurejea Gambia kutoka nchi jirani ya Senegal muda mfupi ujao.
No comments:
Post a Comment