Friday, January 13, 2017

DIMBA LA CHELSEA KUWA KAMA HIVI

Mpango wa Chelsea kujenga uwanja mpya London waidhinishwa

Stamford bridge
Klabu ya Chelsea ya Uingereza imepewa idhini na baraza la wilaya kujenga uwanja mpya mradi ambao utagharimu £500m.
Uwanja huo utakuwa na uwezo wa kutoshea mashabiki 60,000.
Kamati ya mpangilio wa wilaya ya Hammersmith na Fulham imeidhinisha mpango wa kubomoa uwanja wa sasa wa Stamford Bridge unaotoshea mashabiki 41,000.
Miongoni mwa yaliyomo kwenye mpango mpya wa ujenzi, ni pamoja na kujengwa kwa njia ya kutumiwa na watu kutembea kutoka kituo cha reli kilicho karibu.

No comments:

Post a Comment