Saturday, January 21, 2017

TIMU YA WAANDISHI WAHABARI (TPC) YA KUVUTA KAMBA WAIBUKA WASHINDI

 Timu ya kuvuta kamba ya Waandishi wa Habari Tanga Press Club (TPC) wakipeana mbinu kabla ya kuingia katika mchezo wao na timu ya jiji baada ya timu ya Magereza kuingia mitini (kuwakacha) mashindano yaliyofanyika leo na kuandaliwa na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa (RAS) ikiwa ni agizo la Makamo wa Rais kila wiki ya ya pili ya mwezi Taasisi na Mashirika ya Serikali na Umma kufanya mazoezi pamoja na wananchi.
 Waandishi wa habari wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanga Press Club (TPC) Pamela Chaula (mbele) Salma Miraji, Susan Uhinga, Betha Mwambellah, Glory Machaga, na mwisho Katibu wa Tanga Press , Anna Makange, wakivuta kamba dhidi ya timu ya jiji ambapo Tanga Press waliibuka washindi.


 Timu ya kuvuta kamba ya jiji wakiwa katika mtanange ambapo walishindwa na timu ya Waandishi wa habari wa Tanga (Tanga Press Club TPC)





Timu ya waandishi wa habari wa Tanga Press Club (TPC) wakishangilia ushindi dhidi ya timu ya kuvuta kamba ya jiji wakati wa mashindano hayo leo.

No comments:

Post a Comment