Thursday, January 19, 2017

KIPIMO CHA MKOJO KUTAMBUA CHAKULA ULICHOKULA

Wanasayansi wagundua kuchambua ulichokula kupitia mkojo wako

KUNA ugunduzi mpya unaohusu utaalamu wa kupima mkojo wa mwanadamu kupitia maabara na kugundua kila alichokula, kwa mchanganuo wake kamili.

Huo ni utaalamu mpya ulioibuliwa na wanasayansi wa Uingereza na sasa inatarajiwa pindi itapokamilika, itatumika kufuatilia namna mtu anavyokula na viini lishe vilivyomo mwilini mwake.

Hivi sasa hatua iliyoko katika matumizi ya ugunduzi huo ni kwamba, itatumika kuboresha lishe na hasa kwa watu ambao mwenendo wa tabia yao si nzuri hata kidogo na kinyume na maadili ya kuzingatia lishe, ujumbe ukiwafikia hata wenye tabia hiyo au wanaoendekeza ulevi.

Kinachosaidia kuibua ukweli huo ni pamoja na kuchunguza kemikali zilizomo kwenye mkojo, baada ya kupita kwenye mwili wa mwanadamu.

Utafiti unafafanua kwamba picha kamili itapatikana ndani ya miaka miwili ijayo, utafiti utakapofikia hatua nzuri.

Sampuli za mkojo kitabibu hutumika kuchambua muundo wa kemikali iliyomo ndani yake, ili kupata viasharia vya kitabibu.

Watafiti hao wanasema vipomo vya mkojo huo ni mchanganuo wa kina kwa namna mwili unavyoandaa, kile walichokitolea mfano kuwa ni matunda, mboga, samaki na kisha vinaacha viashiria vyake kwenye mkojo.

Wakati ilizoeleka kwenye kinyesi, hilo linawezekana kupitia kwenye mkojo wa mwanadamu.

Ni matokeo ya kazi nzuri kati ya watafiti kutoka Chuo cha Imperial cha London na vyuo vikuu vya Newcastle na Aberystwyth, zote za Uingereza.

Dk. Isabel Garcia-Perez, mmoja wa watafiti hao, anatamka:"Hii hatima yake imetoa kifaa cha kusimamia lishe binafsi na kuweza kusimamia mfumo bora binafsi wa afya.

"Bado hatuko katika hatua kwamba kipimo kikatuambia kwamba mtu alikula chipsi 15 jana na soseji mbili, lakini iko njiani.”

Mwanasayansi mwingine mshiriki wa utafiti kutoka chuo cha Imperial, Profesa Gary Frost, anasema ni utafiti wa kwanza walau kugundua nini anachokula mtu nyumbani.

"Unaweza (daktari) hata kumfafanua mtu kama anafuata masharti ya lishe bora au la. Namna unavyokuwa mkubwa ndivyo inavyokuwa rahisi kufafanua kwenye ripoti juu ya kile unachokula.

"Watu wanaona ni vigumu kugundua kile anachokula nyumbani, jambo ambalo ni tatizo kubwa."

Inaelezwa watafiti hao wanaamini kwamba, vipimo vitasaidia kudhibiti watu kupata vitambi au kukabiliwa na aina ya pili ya kisukari, inayotokana na mfumo binafsi wa maisha kwa mtu.

Profesa Frost anaongeza: "Kama mtu ana mwili mkubwa na anakula vingi na anasema ‘natumia nishati kwa wingi’na vyakula vizito kama vile nyama, kisha utajaribu kubadili mwelekeo na kujaribu tena.

"Imebakia inaangaliwa tu, lakini watu wanaweza kuitikia vizuri na kuna haja kubwa ya kupata chombo hicho kitakachowasaidia wabadilike.”

Anasema,kufanya majaribio yanayohusu kundi kubwa la watu, kunajenga picha kwamba taifa lote ni la walaji na itasaidia kampeni ya kitaifa.

Baada tu ya kuwafanyia majaribio watu 19 ambao wanasimamia lishe zao vizuri na wanasayansi watafiti hao waliweza kubaini tofauti kati ya lishe iliyobeba afya na ile isiyobeba afya.

Watu hao walpewa lishe ya aina nne na kisha mikojo yao ili ikafanyiwe vipimo mara tatu; Asubuhi, mchana na jioni.

Mtaalamu kutoka Baraza la Utafiti wa Afya za Matibabu la Uingereza, Dk. Des Walsh ana maoni:”Kupitia utafiti huu, bado uko katika hatua zake za awali. Bado utafiti uko katika hatua za awali, bado inahangaika na njia muhimu na kula ‘diet’ kunakotakiwa.

"Kupima tunachokula na kunywa kwa usahihi na itakayotupa faida zaidi lishe yetu.”
MGBLOG

No comments:

Post a Comment