Sunday, January 22, 2017

ARSENAL YASHINDA KWA MBINDE DHIDI YA BURNLEY

Alexis Sanchez aliifungia Arsenal bao la piliArsenal yaishinda Burnley mabao 2-1

Alexis Sanchez aliifungia Arsenal bao la pili dakika ya 98 kwa njia ya Penalti na kuiweza kuwashinda Burnley mabao 2-1 Uwanja wa nyumbani Emirates.
Baada ya meneja wa Arsenal Arsene Wenger kutimuliwa uwanjani kwa kulalamikia uamuzi wa refa, kosa la Ben Mee la kumpiga kiatu Laurent Koscielny, lilisabaisha Burnley kuadhibiwa na Arsenal kupewa Penalti.
Arsenal walikuwa wameitawala mechi hadi pale Granit Xhaka alipotimuliwa baada ya kumchezea visivyo Steven Defour, hali iliyosababisha Burnley kunufaika.
Ushindi wa mara tano wa Arsenal katika uwanja wao wa Emirates, unawapandisha jedwali juu na Liverpool na Tottenham, ambao wote walipoteza pointi siku ya Jumamosi na kupunguza mwaya kati yao na Chelsea hadi pointi tano.

No comments:

Post a Comment