HADITHI
ALIYEMUUA MCHUMBA WANGU 20
ILIPOISHIA
James lipopokea simu
alimuuliza.
“James uko kazini au uko
nyumbani?”
“Niko kazini” James alimjibu
kwenye simu.
“Ukitoka mchana kwenda kula
tukutane”
“Si unapafahamu pale
ninapokula?”
“Ndiyo”
“Nikukute hapo”
“Sawa”
Wakati Simon anakata simu
alipata wazo jingine. Upande mmoja wa akili yake ulimwambia arudi pale hoteli
ili aone nini kitatokea. Akageuza gari na kurudi. Alipofika hapo hoteli
aliliegesha gari pembeni.
Tayari alishaona gari la
polisi na gari la hospitali yaliyokuwa yamesimama mbele ya mlango wa hoteli.
Wakati anasimamisha gari aliona polisi waliobeba machela iliyokuwa na mwili wa
Dokta Kweka wakitoka kwenye mlango wa hoteli.
Mwili huo ulipakiwa kwenye
gari la hospitali. Simon alimuona msichana wa Kweka aliyekuwa mke wake
akitolewa na polisi akiwa analia huku mikono yake imefungwa pingu.
Alipakiwa kwenye gari la
polisi. Gari hilo
likaondoka pamoja na gari la hospitali.
Ndipo Simon alipoondoka.
Hakujua ni kwanini mke wake wa zamani alikamatwa, wakati alipofika hapo hoteli
Kweka alikuwa ameshauawa.
SASA ENDELEA
Simon akafikiria kwamba aende Kimara. Kwa vile kile
alichokuwa anakitaka kimetimia aliona aende akajipongeze kwa kinywaji kwenye
baa ya ABC.
Alipofika alilisimamisha gari
kwenye eneo la kuegesha la ABC akashuka na kuingia ndani. Akiwa kwenye ukumbi
wa baa, Simon alizungusha macho kumtafuta kimanzi wake, lakini hakumuona.
Alikwenda kaunta akaketi
kwenye kigoda na kumuuliza msichana aliyemkuta.
“Kimanzi wangu yuko wapi?”
“Anaingia usiku” msichana
huyo alimjibu.
“Oh! Sikufurahi kutomkuta,
nipatie kinywaji”
“Unaweza kumfuata nyumbani
kwake kama unamuhitaji”
“Muda huo wa kufuatana
majumbani ndio sina”
“Basi njoo usiku”
“Nipatie kinywaji”
“Kinywaji gani?”
“Ndiyo tatizo la kutomkuta
Kimanzi, yeye ndiye anayejua kila kitu. Nipatie toti mbili za kunyagi na
kibonge cha barafu”
“Ukija tena kesho nitakuwa
ninajua sasa”
Msichana alimpatia kinywaji hicho.
Simon aliinua bilauli akaipiga funda konyagi iliyopozwa kwa barafu kisha
akaimeza huku akikunja uso.
Aliondoka hapo baa majira ya
saa sita. Ingawa alikunywa konyagi ya kutosha, hakuonesha dalili yoyote ya
kulewa. Alikwenda katika hoteli aliyopanga kukutana na James.
Alipofika alimkuta James
ameshafika.
“Nina habari njema, nataka
kukwambia” Simon aliwambia James huku akiketi.
“Niambie”
“Nimeshamuua Dokta Kweka”
“Sipendi utani Simonai!
“Si utani, tayari nimemuua”
“Umempata
wapi?”
“Nilimuandama na gari hadi
Suzy Hotel, alikwenda kupangisha chumba pale sijui ni kwa ajili gani.
Nikamuingilia chumbani na kumpiga risasi mbili”
James alikuwa akimsikiliza
kwa makini.
“Ilikuwa
saa ngapi?”
“Wakati ule ninakupigia simu
ndiyo ninatoka kumuua”
“Simon una hakika kuwa
umemuua?”
“Amini usiamini. Maiti yake
imechukuliwa na polisi na yule mke wangu alijitokeza pale naye alikamwatwa”
“Alikamatwa kwa sababu gani?”
“Sijajua bado lakini nadhani
ni kwa sababu alikutwa katika eneo la tukio akashukiwa yeye”
“Wakati huo wewe ulikuwa
wapi?”
“Mimi baada ya kumpiga
risasi, nilitoka haraka mle chumbani nikashuka chini na kuingia garini. Nilikaa
kwenye gari kwa muda mrefu, nikamuona yule mwanamke. Alifika pale kwa teksi,
sijui alifuata nini. Akaingia ndani ya hoteli. Baadaye nikaona polisi wamefika”
“Nitakwenda hapo hoteli
kuhakikisha”
“Itakuwa vyema sana, nenda sasa hivi”
“Chakula pia nitasamehe, acha
niende kwanza. Nitakupigia simu nikueleze tukutane wapi. Sawa?”
James alikuwa ameshanyanyuka kwenye
kiti.
“Sawa”
James akatoka na kumuacha
Simon akimtazama.
Dakika chache baadaye
alilisimamisha gari mbele ya hoteli ya Suzy. Mandhari aliyoiona hapo nje ya
hoteli, peke yake ilimuashiria kuwa palikuwa na tukio ambalo halikuwa la
kawaida.
Mbali ya polisi kuendelea kuonekana
katika eneo hilo
kulikuwa na watu waliokuwa wamezagaa mbele ya hoteli.
James alishuka kwenye gari
akaelekea kwenye mlango wa hoteli. Aliwasikia watu wakizungumza kuhusu mtu
aliyeuawa kwa kupigwa risasi ndani ya chumba cha hoteli hiyo.
Aliingia ndani ya hoteli
akaelekea upande wa mkahawa. Kulikuwa na watu wawili watatu wakila chakula
lakini wafanyakazi wa hotelini hapo walionekakana kuwa kwenye taharuki.
James aliketi kwenye meza
iliyokuwa na mtu mmoja.
“Kaka habari ya saa hizi?”
akamsalimia.
“Nzuri. Karibu”
“Asante”
Mhudumu alipomfuata
alimuagiza chakula alichohitaji. Mhudumu alipoondoka alimuuliza yule mtu
aliyemkuta akila chakula.
“Pametokea nini hapa hoteli,
naona watu wengi na polisi?’
“Nilisikia kuna mtu ameuawa
humu ndani” Mtu huyo alimjibu.
James akajifanya anashangaa.
“Kuna mtu ameuawa humu ndani
ya hoteli?”
“Nimesikia aliuawa chumbani, alipigwa risasi
na mtu asiyefahamika”
“Huyo mtu amekamatwa?”
“Hakufahamika”
“Loh! Dar
es Salaam imeharibika sana
siku hizi. Watu wanauana kama nzige!”
“Kwa kweli inatisha sana”
“Na sidhani kama
atapatikana”
“Nimesikia
kuna mwanaamke aliyekamatwa aliyehusishwa na hayo mauaji”
“Mwanamke? Alikamatwa wapi?”
“Hapa hapa hoteli”
Pakapita kimya hadi chakula
alichoagiza James kilipoletwa.
“Eti huyo mtu aliyeuawa hapa
hoteli ni nani?” James akamuuliza mhudumu huyo.
“Alikuwa ni mteja wetu.
Alichukua chumba tangu jana. Leo mchana ndio amekutwa amepigwa risasi chumbani”
Mhudumu huyo akamueleza.
“Alichukua chumba tangu
jana?”
“Ndiyo alikuja jana, hatujui
ni nani aliyemuua na kwa sababu gani”
“Eti kuna mwanamke
aliyekamatwa?”
“Huyo mwanamke ndiye
aliyesababisha tujue kuwa huyo mtu ameuawa. Aliingia mle chumbani kisha akatoka na kupiga
kelele”
“Kwa hiyo siye aliyemuua?’
“Hatujui. Yeye anadai yule
mtu ni mume wake lakini yule bwana alikuja peke yake hapa hoteli”
“Polisi
wamemkamata kwa kumtilia mashaka?” Yule mtu mwingine alisema.
Baada ya hapo mhudumu
aliondoka. James alipomaliza kula alilipa pesa naye akaondoka. Sasa aliamini
kuwa Dokta Kweka alikuwa ameuawa.
“Nitapata mengi kwenye
taarifa ya habari ya usiku” James alijiambia wakati akiendesha gari kurudi
kazini kwake.
**************
Alikuwa mfanyakazi mmoja wa
hoteli ya Suzy aliyeitwa Mage ambaye alimpigia simu Vicky na kumjulisha kuwa
mwanaume wake alikuwa amepangisha chumba hapo hoteli.
Vicky ambaye alikuwa mke wa
Simon kabla ya kuchukuliwa na Dokta Kweka alikuwa akifahamiana na Mage na
ulikuwa umbea tu wa kike uliomfanya Mage ampigie simu.
ITAENDELEA
|
1:14 AM (8 hours ago)
|
|
Translate message
Turn off for: Swahili
HADITHI
ALIYEMUUA MCHUMBA WANGU 22
ILIPOISHIA
“Ndiyo alikuja jana, hatujui
ni nani aliyemuua na kwa sababu gani”
“Eti kuna mwanamke
aliyekamatwa?”
“Huyo mwanamke ndiye
aliyesababisha tujue kuwa huyo mtu ameuawa. Aliingia mle chumbani kisha akatoka na kupiga
kelele”
“Kwa hiyo siye aliyemuua?’
“Hatujui. Yeye anadai yule
mtu ni mume wake lakini yule bwana alikuja peke yake hapa hoteli”
“Polisi
wamemkamata kwa kumtilia mashaka?” Yule mtu mwingine alisema.
Baada ya hapo mhudumu
aliondoka. James alipomaliza kula alilipa pesa naye akaondoka. Sasa aliamini
kuwa Dokta Kweka alikuwa ameuawa.
“Nitapata mengi kwenye
taarifa ya habari ya usiku” James alijiambia wakati akiendesha gari kurudi
kazini kwake.
**************
Alikuwa mfanyakazi mmoja wa
hoteli ya Suzy aliyeitwa Mage ambaye alimpigia simu Vicky na kumjulisha kuwa
mwanaume wake alikuwa amepangisha chumba hapo hoteli.
Vicky ambaye alikuwa mke wa
Simon kabla ya kuchukuliwa na Dokta Kweka alikuwa akifahamiana na Mage na
ulikuwa umbea tu wa kike uliomfanya Mage ampigie simu.
SASA ENDELEA
“Mwanume wako amechukua
chumba hapa hoteli, sijui ana mwanamke” alimwambia.
Vicky kusikia ile taarifa akashituka.
“Amechukua chumba muda huu?”
“Alifika tangu jana hapa
hoteli akachukua chumba na anaendelea nacho hadi leo”
“Inawezekana yuko na mwanamke
wake, ngoja nije hapo hapo”
“Basi wahi, usichelewe”
“Nakuja sasa hivi”
Ndipo Vicky alipokodi teksi
iliyompeleka Suzy Hotel. Mwenyeji wake alimwambia kuwa mwanaume wake alikuwa
chumba namba 45. Vicky akapanda ngazi haraka haraka akiamini kuwa alikuwa
anakwenda kufumania.
Alipofika kwenye mlango namba
45 aliufungua na kuingia ndani, ndipo alipoiona maiti ya Kweka aliyekuwa
amepigwa risasi mbili za kifua. Akatoka mbio huku akipiga kelele.
Wafanyakazi wa hoteli
walipomuuliza”Kulikoni?” ndipo akaeleza kuwa mume wake alikuwa ameuawa
chumbani.
Baada ya maiti ya Kweka
kuonekana mle chumbani ndipo uongozi wa hoteli ulipopiga simu polisi. Polisi
wakafika na mshukiwa wa kwanza akawa ni Vicky.
Akiwa kituo kikuu cha polisi
Vikcy alikuwa akiendelea kulia.
Afisa wa polisi Inspekta
Temba alimtaka anyamaze ili waweze kuchukua maelezo yake.
“Unaitwa nani” alimuuliza.
“Naitwa Vicky Benjamin”
“Una umri gani?”
“Miaka 30”
“Marehemu alikuwa nani wako?”
“Alikuwa mume wangu”
“Una uthibitisho wowote kuwa
alikuwa mume wako?”
Vicky alimuonesha Inspekta
Temba picha alizopiga akiwa na Dokta Kweka kwenye simu.
“Uligunduaje kuwa Kweka
alikuwa ameuawa?”
“Nilifika pale hoteli
kumfuata yeye, niliambiwa kuwa alikuwa amechukua chumba…”
“Uliambiwa na nani?”
“Niliambiwa na rafiki yangu
mmoja anayefanya kazi pale”
“Yeye ndiye aliyekwambia kuwa
marehemu alikuwa amechukua chumba?”
“Ndiyo”
“Anaitwa nani huyo mtu
aliyekwambia?”
“Ni msichana, anaitwa Rose”
“Alikwambia mume wako alichukua
chumba kwa ajili gani”
“Yeye hakujua, isipokuwa
alishuku kwamba huenda alikuwa na msichana”
“Okey. Kwa hiyo wewe
ulikwenda pale hoteli kwa hisia kwamba mume wako alikuwa na msichana?”
“Ndiyo”
Inspekta Temba alinyamaza kwa
muda kutafakari kabla ya kuuliza swali jingine.
“Ulipofika pale hoteli
ulikutana na marehemu”
“Hapana, nilikuta maiti yake
tu”
“Hukukuta msichana yeyote?”
“Alikuwa peke yake chumbani”
“Hukuona dalili yoyote ya
kuwemo msichana?”
“Sikuchunguza, nilipoona
marehemu yupo chini nilitoka na kupiga kelele”
“Kwa kadiri ulivyokuwa
unaijua tabia ya mume wako, alikuwa na msichana nje”
“Sina hakika na jambo hilo” Vicky alijibu kwa
kusitasita.
“Sawa. Tutaendelea
kukushikilia kama mshukiwa namba moja hadi
hapo tutakapokamilisha uchunguzi wetu”
“Sasa mimi nashikiliwa kwa
kosa gani?”
“Mazingira ya kuweko kwako
katika eneo la tukio yanaitia shaka polisi. Tutakapojiridhisha kuwa maelezo
uliyotupa ni ya kweli tutakuachia”
“Mimi siwezi kumuua mume
wangu na pia sina bastola”
“Ni shaka tu tuliyonayo sisi
polisi, acha tuendele na upelelezi wetu”
Inspekta Temba akamuagiza
polisi mmoja mwanamke akamuweke ndani Vicky.
Baada ya Vicky kuwekwa ndani
Temba alitoka na gari akaenda Suzy Hotel. Alikwenda mapokezi na kukutana na
msichana ambaye alimpokea Dokta Kweka alipofika hapo hoteli kukodi chumba.
“Jina lako nani?’ alimuuliza.
“Naitwa Fatuma Amraan”
“Wewe ndio ulimpokea Kweka
alipofika hapa hoteli?”
“Ndiyo, mimi ndiye
niliyemuandikisha”
“Kweka alikuja lini hapa”
“Alichukua chumba tangu jana”
“Alilala hapa?”
“Sina hakika kwa sababu
sikuwepo usiku”
“Hebu niambie alikuwa na
mwenzake yeyote?”
“Alikuwa peke yake”
“Hakuwa na msichana?”
“Sikuona msichana”
“Yuko wapi Rose?”
“Rose yupo, ngoja nimuite”
Alimuita kwa kumpigia simu ya
mkononi.
“Rose unaitwa hapa kaunta”
“Naitwa na nani?” Sauti ya
Rose ikauliza kwenye simu.
“Kuna askari anakuulizia”
“Anataka nini?”
“Sijui, we njoo umsikilize.
Si unajua kuna tukio limetokea hapa hoteli”
“Mimi bado nina kazi”
“Njoo mara moja”
Fatuma akakata simu. Dakika
chache baadaye Rose akafika hapo mapokezi. Alimsalimia Inspekta Temba kisha akamuuliza Fatuma.
“Nani
ananiita?”
“Nimekuita mimi” Inspekta
Temba alimwambia na kuongeza.
“Naitwa Inpekta Temba,
natokea makao ya polisi. Wewe ndiye Rose?”
“Ndiye mimi”
“Unamfahamu Vicky?”
“Namfahamu?”
“Ni kweli kwama mtu aliyeuawa
hapa hoteli ni mume wake?”
“Ndio, ni mume wake”
“Wewe ndio ulimpigia simu
kumjulisha kuwa mume wake amekodi chumba hapa hoteli”
Rose akagwaya.
“Nataka jibu”
ITAENDELEA hapaha pa usikose uhondo hu
No comments:
Post a Comment