Tuesday, January 24, 2017

ASHITAKIWA KUENDESHA GARI AKIWA AMESIMAMA

Ashtakiwa kwa kuendesha gari akiwa amesimama

Ashtakiwa kwa kuendesha gari akiwa amesimama
Adam ElliottMtu anaedaiwa kuwa mrefu ameshtakiwa kwa kuendesha gari akiwa amesimama baada ya kukiri kupeleka gari vibaya.
Adam Elliott alituhumiwa kwa kuwaonyesha madereva wengine kichwa chake kikiwa kinaonekana juu ya paa la gari hilo aina ya Ford Ka.
Elliott mwenye umri wa miaka 26 kutoka mji wa Newcastle, ambaye ana urefu wa mita mbili alikiri kufanya makosa hayo katika mahakama ya Newcastle lakini akalaumu urefu wake.
Akizungumza baada ya kesi hiyo, alisema: Sikuwa nimesimama, mimi ni mrefu ndio maana.
Jaji Robert Adams alisema kuwa ni wazi kwamba Adam alitaka kuonekana akiendesha gari akiwa amesimama ili kuonyesha urefu wake.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment