Friday, January 27, 2017

JICHO LA MCHEZAJI WA MPIRA WA KIKAPU LATOKA AKIWA UWANJANI

Jicho la mchezaji latoka akiwa uwanjani

JANUARY 26: Akil Mitchell
Mchezaji wa mpira wa kikapu nchini New Zealand Akil Mitchell amesema anapata nafuu baada ya jicho lake kutoka alipokuwa uwanjani akicheza.
Mitchell huchezea klabu ya New Zealand Breakers, na alikuwa mjini Auckland kucheza mechi ya NBL ya Australia Alhamisi usiku kisa hicho kilipotokea.
Mchezaji wa timu pinzani aliingiza kimakosa kidole ndani ya tundu la kishimo cha jicho na ghafla jicho lake likatoka nje.
Mchezaji huyo mzaliwa wa Marekani alianguka sakafuni akiwa ametumia mikono yake kufunika jicho lake la kushoto na akakimbizwa hospitalini.

No comments:

Post a Comment